Mark 6:14-19

14 aMfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Isa lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yahya Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

15 bWengine wakasema, “Yeye ni Ilya.”

Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.”

16 cLakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yahya Mbatizaji, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!”

17 dKwa kuwa Herode alikuwa ameagiza kwamba Yahya Mbatizaji akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, ambaye Herode alikuwa amemwoa. 18 eYahya alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.” 19Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yahya kinyongo akataka kumuua. Lakini hakuweza,
Copyright information for SwhKC